Saturday, August 17, 2019

Piga mkwanja wa Ligi Kuu England wikiendi hii

Tags

Mechi hizo pia zinatoa fura ya kupiga mkwanja kwakutabiri matokeo ya michezo kadha wa kadha. Opera News itakuwa ikikuletea michezo mitatu ya kutabiri kila wikiendi. Sasa wikiendi hii tunaanza na michezo hii.
Arsenal VS Burnley(Jumamosi)
Image result for aubameyang
Arsenal almaarufu Washika Bunduki walishinda mchezo wao wa ufunguzi ambao walikuwa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Newcastle. Jambo la kuvutia zaidi, kocha Unai Emery hakuwa na nyota wake Mesut Ozil pamoja na beki wake wa kushoto Sead Kolasinac wakati huo huo akimpumzisha mshambuliaji wake hatari Alexandre Lacazette.
Kwa upande wao, Burnley wakiwa nyumbani waliwaadhibu Southampton magoli 3-0 na kuwa mbele ya Arsenal kwenye msimamo wa ligi. Hata hivyo hawajawahi kuwafunga Arsenal ndaniya mechi 5 za mwisho walizokutana.
Alama za kutabiri: Arsenal wamepewa @1.36 za kushinda
Everton-Watford(Jumamosi)
Image result for everton
Mechi iliyopita walitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Leicester City na watakuwa wakihitaji ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wao katika uwanja wa nyumbani wikiendi hii. Everton maarufu ‘The Toffees’ wana timu nzuri kiasi na msimu uliopita walipata matokeo ya kuridhisha mbele ya baadhi ya wababe, Arsenal walipigwa 3-0 huku United wakichakazwa 4-0!
Wakati huo huo, Watford walishuhudia wakipokea kipigo kizito nyumbani msimu uliopita mbele ya Brighton ambao wameshuka daraja cha mabao 3-0.
Alama za kutabiri: Everton wamepewa @1.73 za kushinda
Manchester City-Tottenham Hotspurs(Jumamosi)
Image result for raheem sterling
Mabingwa hao watetezi wamethibitisha kwamba bado wana kiu ya ubingwa kwa kuwafunga West Ham mabao 5-0 katika dimba lao la nyumbani la London Stadium. Raheem Sterling alipiga hat-trick katika mchezo huo ambao vijana wa Pep Guardiola walitawala vilivyo.
Tottenham waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wageni Aston Villa waliopanda daraja msimu huu. Historia inawabana Spurs kwani hawajawahi kupata matokeo ya ushindi Etihad mbele ya Pep Guardiola.
Alama za kutabiri: Manchester City wamepewa @1.36 za kushinda