NIYONZIMA KUWAKOSA KMC DAR..

Image may contain: 1 person, playing a sport and outdoor

Klabu ya As Kigali ya Rwanda imethibitisha kuwa Kiungo wao Fundi na nahodha wa klabu hiyo Haruna Niyonzima ataukosa mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya KMC FC mchezo ambao utachezwa siku ya Ijumaa ya August 23 katika dimba la Taifa, Dae kwa kiingilio cha 2000 tu.

Sababu kubwa ambayo inamfanya kiungo huyo wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga kukosekana ni kuchelewa kupata leseni yake kutoka CAF yeye na Ndayishimiye Eric Bakame. Ila As Kigali imesema itasafiri naye kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo huo.
MaoniMaoni Yako