Ninja aanza rasmi kukipiga na Zlatan Ibrahimovic

Ninja aanza rasmi kukipiga na Zlatan
Ninja aanza rasmi kukipiga na Zlatan
BEKI Abdallah Shaibu 'Ninja' ametambulishwa katika klabu yake mpya ya LA Galaxy inayoshiriki Ligi kuu ya Marekani (MSL) iliyo na nyota kadhaa wa straika wa zamani wa Man United, Zlatan Ibrahimovic.
Ninja aliyekuwa anaichezea Yanga msimu uliopita, amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Akiwa kikosi cha Yanga alikuwa muhimili mkubwa katika safu ya ulinzi baada a kuanza kukopi akiwa na Andrew Vincent au Kelvin Yondani.
Pia uwezo wake wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji kulimfanya awe anapata nafasi ya kuanza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
Usajili wake katika kikosi cha LA Galaxy kutamfanya acheze na mshambuliaji Zlatan nyota awa zamani wa kimataifa wa Sweden aliyewahi kutamba na klabu mbalimbali Ulaya ikiwamo Barcelona, PSG na Manchester United.
MaoniMaoni Yako