Saturday, August 17, 2019

Namungo Wataja Kilichowaponza Kupokea Kichapo Cha Mabao 8-1 Mble Ya Azam Fc

Tags

Namungo Wataja Kilichowaponza Kupokea Kichapo Cha Mabao 8-1 Mble Ya Azam Fc

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kilichoiponza timu yake kupokea kichapo kibaya cha mabao 8-1 ni kukosa uzoefu pamoja na muunganiko wa timu.

Namungo yenye maskani yake Lindi, ilifungwa mabao 8-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Chamazi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa ni kipigo kibaya ambacho wamekipata hasa kwenye mechi ya maandalizi hivyo makosa waliyofanya watayatafutia dawa.

"Haikuwa jambo jema kwetu kupokea kichapo cha mabao yale, ila sababu kubwa ni kutokuwa na maandalizi hasa kwa wachezaji wapya ambao wamejiunga na kikosi, tayari tumeanza kufanyia kazi mapungufu hivyo wakati ujao tutafanya vizuri kwani kwenye mpira chochote kinatokea," amesema.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Azam FC lilipachikwa na mpigaji wao mipira iliyokufa Kikoti.