Namungo FC yawatuliza Mashabiki

Namungo FC yawatuliza Mashabiki
Namungo FC yawatuliza Mashabiki

HITIMANA Thiery Kocha Mkuu wa Namungo FC amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kwa kusema kuwa timu bado ina nafasi ya kuleta ushindani msimu ujao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa mechi za maandalizi zimewapa fursa ya kutambua makosa yao jambo litakalowafanya wawe bora msimu ujao.

“Kichapo cha mabao mengi kimekuwa kibaya kwetu, tayari tumeanza kujipanga kufanya vema msimu ujao kwa kuwa makosa tumeyaona na tunayafanyia kazi.

“Tuna muda wa siku nne za maandalizi, zinatosha kusuka upya kikosi chetu ninawaomba mashabiki wasiwe na mashaka kwani kila kitu kinawezekana,” amesema Thiery.

Mchezo wa kwanza wa Namungo kwenye Ligi Kuu Bara utakuwa Agosti 24 na itamenyana na Ndanda FC ya Mtwara uwanja wa Majaliwa.

Inashikilia rekodi ya kuchapwa mabao mengi kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kwnye michezo ya kirafiki ambapo ilipoteza kwa kufungwa mabao 8-1dhidi ya Azam FC.
MaoniMaoni Yako