Naldo, Chirwa, Ngoma pasua kichwa Azam

Naldo, Chirwa, Ngoma pasua kichwa Azam

IDD Chehe, Kocha Msaidizi wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa tatizo kubwa ambalo ni pasua kichwa kwa sasa ndani ya kikosi hicho ni umaliziaji wa nafasi wanazotengeneza.

Azam FC inashiriki michuano ya kimataifa na itacheza na Kenema ya Ethiopia Agosti 10 nchini Ethiopia kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mwisho.

Safu ya ushambuliaji inaundwa na Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Iddy Suleman 'Naldo' na Khasim Khamis kwa sasa.

"Tatizo kubwa kwa timu lipo kwenye umaliziaji wa nafasi ambazo tunatengeneza hivyo hilo ndilo tunalifanyia kazi kwa ukaribu ili kumaliza kabisa hilo tatizo," amesema.