Mziki wa Yanga wamkuna Rc Hapi

Mziki wa Yanga wamkuna Rc Hapi

UKISIKIA chuzi limekolea nazi ndio Yanga ya sasa, kwani mpaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amekubali na kukiri kwamba kwa msimu, timu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali na wapinzani wa klabu hiyo wajipange mapema wasiaibike.
Hapi aliyekuwepo uwanjani wakati wa mchezo wa Yanga  jana dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya katika kilele Cha Wiki ya Mwananchi', alisema usajili uliofanywa Jangwani na jinsi alivyoona wachezaji hao wanavyocheza anaamini timu hiyo itakuwa moto mno.
Mkuu huyo wa mkoa ambaye pia ni shabiki kindaki ndaki wa Yanga amefurahishwa na viwango vya wachezaji wapya wa timu hiyo huku pia kiafurahia viwango vya wachezaji wa zamani.
"Nimefurahi kuona timu imecheza vizuri sana na kuonyesha kuwa msimu ujao tutakuwa Moto na hakuna wa kutugusa. Baadhi ya wachezaji wameonekana kupandisha viwango vyao  lakini pia wachezaji wapya kama Sadney Ukhrob,Juma Balinya na Patrick Sibomana wameonyesha uwezo mkubwa utakaokuwa msaada kwa timu hii na kutwaa ubingwa."
Pia Hapi amewapongeza mashabiki wa Yanga kwa kuujaza Uwanja wa Taifa na kuwataka kufanya hivyo kila mechi iku kuwapa hamasa wachezaji.
"Leo Uwanja umefurika,inapendeza Sana na tusiishie hapa bali kila mechi iwe ya ligi au ya kimataifa mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kuwapa sapoti wachezaji ili nao watuletee ushindi.
Yanga ilihitimisha Wiki ya Mwananchi kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa klabu hiyo mwaka 1935 ikiwa ni mwanzo wa kuanza msimu mpya wa mashindano wa mwaka 2019-2020 ambapo timu hiyo itashiriki Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.
MaoniMaoni Yako