Monday, August 12, 2019

Mrithi wa Makambo Yanga huyu hapa

Tags

Mrithi wa Makambo Yanga huyu hapa
MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wale ambao wanabeza uwezo wa mshambuliaji wake mpya, David Molinga watamuelewa tu ligi ikianza.

Molinga ni mshambuliaji mpya wa Yanga ambaye amejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea AC Lega ya Congo kuchukua mikoba ya Heritier Makambo ambaye ametimkia AC Horoya.

Zahera amesema kuwa, wengi wanabeza uwezo wake kutokana na kuona hafungi mabao ila siku moja watamuelewa tu.

“Alikuwepo Makambo, walimsema baadaye wao wakakaa kimya kwa majibu yake uwanjani, hivyo kwa sasa ni zamu ya Molinga kuwaonyesha kile alichonacho.

“Kwa sasa anashindwa kuonyesha makeke kutokana na ukweli kwamba yeye alichelewa kuungana na wachezaji kwenye maandalizi ya awali, ila nina uhakika na kile alichonacho watamuelewa tu,” amesema.