Saturday, August 3, 2019

Michezo ya majeshi kutimua vumbi Nairobi Agosti 12, JWTZ kupeleka 105

Tags

Michezo ya majeshi kutimua vumbi Nairobi Agosti 12, JWTZ kupeleka 105
MICHUANO ya Majeshi katika nchi sita za Afrika, yanatarijiwa kuaanza kutimua vumbi Agosti 12 hadi 24 mwaka huu, mjini Nairobi nchini Kenya huku Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likitarajia kupeleka viongozi na wachezaji 105.


Katika kuhakikidha Tanzania inashiriki kikamilifu michuano hiyo, Benki ya NMB imetoa udhamini vifaa vya michezo ikiwamo jezi na mipira vyenye thamani ya Sh. milioni 15.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Brigedia Jenerali, David Mallugu, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo leo jijini humo, amesema JWTZ inapeleka washiriki wa michezo mitano.

Ametaja michezo watakayoshiriki ni mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, riadha na mbio za magongo.

"Tunaishukuru NMB kwa kuendelea kutudhamini katika michuano hii muhimu kwetu sisi, tunaahidi tutarudi na ushindi wa jumla, la sivyo tutarudi na vikombe vingi zaidi kwa sababu tumejiandaa kikamilifu kwa kupeleka timu za michezo mingi tofauti na nchi nyingine," Brigedia Jenerali Mallungu amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Huduma Binafsi wa NMB, Omary Mtiga, amesema ni mara ya nne benki hiyo inaendelea kufadhili michuano hiyo ya majeshi.

Amesema wanawatakia kila la heri katika michuano hiyo huku wakiamini kuwa timu hiyo itarudi na ushindi hivyo kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.