Monday, August 12, 2019

Messi apigania namba mechi yao dhidi ya Athletic Bilbao

Tags

Messi apigania namba mechi yao dhidi ya Athletic Bilbao
LIONEL Messi staa wa Barcelona ameanza mazoezi ya Gym ikiwa ni sehemu ya matibabu yake kufuatia majeraha aliyoyapata hivi karibuni.

Messi aliumia mara baada ya kuripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo inayojiaandaa na msimu ujao wa 2019/20.

Kufuatia hali hiyo ameshindwa kusafiri na timu hiyo kwenda Marekani ambako ilikwenda kwa mechi za kirafiki.

Messi anakabiliwa na maumivu ya mguu ambayo yanaweza kumfanya kukosa mechi za mwanzo za msimu.

Messi anapambana kuwa fiti ili kurejea kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Athletic Bilbao, Agosti 16 mwaka huu.