Saturday, August 17, 2019

Mbrazil aliyekipiga na Neymar Jr, Coutinho amapa tano Mbelgiji wa Simba

Tags

Mbrazil aliyekipiga na Neymar Jr, Coutinho amapa tano Mbelgiji wa Simba
BEKI mpya wa Simba, raia wa Brazil, Gerson Vieira Fraga, amemtaja kocha mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems, kuwa ni wa kipekee.

Vieira amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa U17 ya Brazil, iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson Becker wa Liverpool, amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kukipiga Msimbazi akitokea katika Klabu ya ATK FC ya India.

Vieira amesema anafurahi kuona yupo kwenye timu bora yenye wachezaji wengi wazuri wanaompa changamoto ya kupambana lakini kikubwa ni uwezo alionao kocha Aussems katika kufundisha soka.

Leo Simba itakuwa na kibarua mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 Usiku.