Mbelgiji wa Simba awapa mapumziko wachezaji wake

Mbelgiji wa Simba awapa mapumziko wachezaji wake
WACHEZAJI wa Simba leo kazi ni kwao kuamua kula bata ama kupumzika na familia zao nyumbani ama kwenda kwa ndugu na majamaa.

Ruksa hiyo ni baada ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems kuwapa mapumziko ya siku moja baada ya kutoka kupeperusha Bendera ya Kimataifa nchini Msumbiji.

Aussems amesema ni muhimu kwa wachezaji kurejea nyumbani na kupata mapumziko wakiwa na familia ili kujenga uwezo mpya watakaporudi kuanza maandalizi ya michezo yao inayofuata.

Kibarua cha kwanza itakuwa ni Jumamosi Uwanja wa Taifa ambapo Simba itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa ngao ya jamii kabla ya kurudiana na UD Songo ya Msumbiji kati ya Agosti 23-25 Bongo.
MaoniMaoni Yako