Mavugo Ashindwa Kung'aa Tanzania, Atamba Zambia


Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC raia wa Burundi Laudit Mavugo anayekipiga Napsa FC ya nchini Zambia wikiendi iliyopita amekabidhiwa tuzo yake ya mfungaji bora wa Ligi Kuu nchini Zambia msimu wa 2018/2019.

Mavugo amekabidhiwa tuzo hiyo akiwa pamoja na washambuliaji wengine wawili Austin Muwowo na Zikiru Adams kwa kufungana kwa kufunga magoli 10 kila mmoja, Mavugo pia ameingia katika kikosi bora cha Ligi Kuu Zambia cha msimu wa 2018/2019.

Laudit Mavugo anaibuka mfungaji bora Zambia ikiwa ndio msimu wake wa kwanza katika Ligi hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Burundi aliondoka Simba Disemba 2017 baada 
MaoniMaoni Yako