Mashabiki wa SIMBA Wavunja Record Kwa Kununua Viti Vyote 60,000 Uwanja wa Taifa

Mashabiki wa SIMBA Wavunja Record Kwa Kununua Viti Vyote 60,000 Uwanja wa Taifa
Mashabiki wa Simba wakomba tiketi zote za SportPesa Simba Wiki

Mashabiki wa klabu ya Simba wamedhihirisha ubingwa wao leo na kuweka rekodi ya kujaza uwanja wa Taifa kwa kuuza tiketi zote 60,000 za SportPesa Simba Wiki ambayo imekamilika siku ya leo.

Zilianza kumalizika tiketi za mzunguko ambazo zilikuwa zinauzwa 5,000 (buku tano) kabla ya nyingine ambazo zilikuwa zinauzwa 150,000 kwa Platinum, 100,000 Platinum, VIP A 30,000, VIP B na C 15,000 nazo pia zikaisha.

Hivyo Simba wameweka rekodi ya kuuza tiketi zote ambazo waliziandaa kwenye mchezo wa leo wa kimataifa dhidi ya Power Dynamo ambapo wameibuka na ushindi wa mabao 3-1.
MaoniMaoni Yako