Monday, August 19, 2019

MASHABIKI WA SIMBA WAONYESHA UUNGWANA

Tags

Tokeo la picha la MASHABIKI WA SIMBA
Juzi video ya mashabiki wa Yanga mkoani Kilimanjaro ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii wakichana jezi ya klabu ya Simba tukio ambalo lilikemewa vikali na familia ya soka nchini ukiwemo uongozi wa Yanga ambao uliwataka mashabiki wao kuacha tabia ya kufanya uhasama kwenye ushabiki

Lakini mwenzao wa Simba wamewafundisha kuwa Simba na Yanga ni watani tu na hakuna uhasama wowote baina yao baada ya hapo jana baadhi ya mashabiki kumkaribisha mshambiki wa Yanga aliyekuwa akishangilia Azam Fc kukaa jukwaa la Simba


Tukio hilo lilitokea kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc na kumfanya shabiki huyo ajikute kwenye wakati mgumu baada ya kupigo hicho cha Azam