Martin Kadinda Afunguka Kuhamia Kwa Hamisa Mobetto

Martin Kadinda Afunguka Kuhamia Kwa Hamisa Mobetto
MWANAMItINdo wa kiume Bongo, Martin Kadinda amefungukia madai ya kuhamia na kumsimamia mwanamitindo Hamisa Mobeto kuwa alikuwa akifanya mambo ya kishikaji na siyo kwamba yuko kwake sasa hivi. Akizungumza na Za Motomoto, Kadinda alisema kuwa yeye na Hamisa mara nyingi wanapata mialiko

mbalimbali kwenye mashindano ya urembo na mrembo huyo aliomba tu amsaidie kutoka naye nje mpaka kwenye gari lake wakati lilipomalizika shindano la Miss Kinondoni hivi karibuni. “Watu wana maneno Hamisa, yeye aliniomba tu nimsindikize nje mpaka kwenye gari lake na siyo kwamba sasa hivi nafanya kazi kwake na kamkacha Wema kitu ambacho sicho,” alisema Kadinda