Manchester United Yalaani Pogba Kubaguliwa


Klabu ya Manchester United imelaani vikali kitendo cha ubaguzi wa rangi dhidi ya kiungo Paul Pogba baada ya mechi ya juzi usiku dhidi ya Wolverhampton.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 alikabiliwa na kitendo hiko baada ya kukosa penati dakika ya 68 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Wolverhampton uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Manchester United wamesema kwamba wamechukizwa na kitendo hiko na watachukua hatua kali dhidi ya wahusika wa kitendo hiko cha ubaguzi wa rangi.

"Kila mtu ndani ya United amechukizwa na kitendo hiko cha ubaguzi wa rangi dhidi ya Pogba jana usiku na tunalaani vikali kitendo hiko" imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na klabu ya Manchester United.
MaoniMaoni Yako