Manara Awataka Mashabiki Simba Kuziunga Mkono KMC Na Azam Huku Akiwataka Waiombee Dua Yanga Licha Ya Kua Ni Ngumu Kufanya Hivyo...Haji Manara:- Nimekubaliana na C.E.O mechi ya KMC tunakwenda na tunaomba wana Simba wote twende, mechi ya Jumamosi na Azam tunakwenda Chamazi na tunaomba wana Simba na Watanzania wote twende kama itakavyokuwa Jumapili .
.

Lakini pia kuwaombea kheri Yanga ambao wanacheza kule Gaboroni siku ya Jumamosi
Ni ngumu kuiombea dua Yanga, ngumu, ngumu katika vigumu Duniani ni kuwaombea dua Yanga hasa dua la kheri .
.

Lakini si Watanzania hawa na wanawakilisha Nchi, kwasababu pale Bendera inapanda pale ya Tanzania ya Caf, Botswana, bendera yetu ipo kule
Ingawa siku hizi katika utamuduni wa sasa hivi vilabu vikubwa havipigiwi nyimbo za Taifa lakini bado wale ni wakilishi wa Tanzania
MaoniMaoni Yako