Saturday, August 17, 2019

Lukaku Aipiga Dongo Manchester United

Tags

Lukaku Aipiga Dongo Manchester United
ROMELU Lukaku, mshambuliaji mpya wa kikosi cha Inter Milan ametupa dongo kimtindo kwa timu yake ya zamani ya Manchester United alipokuwa akitoa mlinganisho wa mazoezi akiwa na kikosi chake kipya.

Lukaku amenukuliwa akisema kuwa alipokuwa England mazoezi yalikuwa ni mengi lakini Inter Milan kuna mazoezi ya ukweli kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni dongo kwa Manchester United iliyo chini ya Ole Gunnar Solkjaer.

"Hapa mazoezi ni magumu, kule England kazi ni nyingi na lakini huku kuna mazoezi ya ukweli," amesema.