Saturday, August 10, 2019

Lori la Mafuta laua Watu 57 Morogoro

Tags

 Lori la Mafuta laua Watu 50 Morogoro

Morogoro. “Inasikitisha”. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Agosti 10, 2019 ambapo Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia miili iliyoungua ikiwa imelazwa pembeni ya barabara ya  Dar es Salaam-Morogoro wengi wakiwa ni madereva bodaboda na mamalishe wanaofanya shughuli zao hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi.

Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.

Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.

Wamesema mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alikuwa akivuta sigara, kwamba ndio chanzo cha mlipuko huo.

Pia Soma