Monday, August 12, 2019

Kuwaona wa kimataifa Simba na Azam Fc Taifa 5000/= tu

Tags

Kuwaona wa kimataifa Simba na Azam Fc Taifa 5000/= tu
Kuwaona wa kimataifa Simba na Azam Fc Taifa 5000/= tu
MCHEZO wa Ufunguzi wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC na Simba unatarajiwa kupigwa Agosti 17 uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ni wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23 ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Mabingwa watetezi Simba na JKT Tanzania uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF'  Clifford Ndimbo amesema kuwa kiingilio kwenye mchezo huo kwa jukwaa la mzunguko ni 5,000 na Jukwaa la VIP B na C itakuwa 10,000.

Mchezo wa ngao ya Jamii huwakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambao ni Simba pamoja na mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Azam FC.