Kutoka Azam FC


Anaitwa Richard Djodi mwamba wa Azam FC kutoka nchini Ivory Coast, yuko tayari na jeshi zima la timu hiyo kuifanyia mauaji Fasil Kenema Jumamosi hii saa 10.00 jioni.

Anachoomba kutoka kwako, ni mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kuwashangilia kwenye Uwanja wa Azam Complex, ili waweze kupata nguvu ya kuwaua Wahabeshi.

Mbali na zawadi ya Azam Ukwaju ya Bureee kwa kila shabiki mlangoni, wachezaji wa Azam FC wamepanga kuwapa zawadi nyingine mashabiki watakaojitokeza uwanjani na Watanzania kiujumla, na hii si nyingine ni ushindi utakaoiwezesha kusonga mbele kwa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam FC ni ya Tanzania. Tanzania ni ya Watanzania. Twendeni kwa wingi tukawasapoti Watanzania wenzetu Jumamosi. 
MaoniMaoni Yako