Saturday, August 17, 2019

Kocha Yanga Ataja Sababu Ya Kichapo Cha Mabao 2-0 Mbele Ya Polisi Tanzania

Tags

Kocha Yanga Ataja Sababu Ya Kichapo Cha Mabao 2-0 Mbele Ya Polisi Tanzania
MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kupoteza mchezo wake mbele ya Polisi Tanzania ni kukosa umakini kwa wachezaji wake kwenye mchezo huo.

Jana Yanga ilipoteza mchezo wake mbele ya Polisi Tanzania ulochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi kwa kufungwa mabao 2-0 ambao ulikuwa wa kirafiki.

Mabao ya Polisi Tanzania yalifungwa na Marcel Kaheza pamoja na Ditram Nchimbi na kuifanya Polisi kuibuka wababe kwenye mchezo huo.

Zahera amesema,:"Ulikuwa ni mchezo mzuri na mgumu, kila timu ilikuwa inapambana kutafuta matokeo chanya mwisho wa siku wachezaji wangu wameshindwa kuwa makini kutumia nafasi walizozipata na kuruhusu kufungwa, wakati mwingine tutaongeza umakini kupata matokeo," amesema.