Kocha Singida United aanza kutema cheche

Kocha Singida United aanza kutema cheche
FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Singida United amesema kuwa kazi itakuwa moto msimu ujao kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Minziro amesema kuwa timu inaendelea na maandalizi mkoani Mwanza kwa ajili ya msimu ujao.

"Timu ipo sawa kila kitu kinakwenda vizuri, wachezaji wanapambana na wanakazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya msimu ujao.

"Ushindani utakuwa mkubwa nasi pia tumejipanga kufanya vizuri kikubwa sapoti kutoka kwa mashabiki na wadau" amesema.
MaoniMaoni Yako