KMC Yatupwa Nje Michuano Ya CAFKMC imekuwa timu ya Kwanza ya Tanzania kuondolewa kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kuchapwa mabao 2-1 na AS Kigali ya Rwanda.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, KMC itabidi ijilaumu kwa kiwanho chake kibovu kilichopelekea kupata matokeo hayo.

Mabao ya AS Kigali katika mchezo wa leo yamefungwa na Rashid Kalisa na Erick Nsabimana wakati la KMC limefungwa na Yusuph Ndikumana kwa penalti.

KMC ambayo ni mara ya kwanza inashiriki mashindano hayo, ilicheza vibaya hasa eneo la ulinzi na ushambuliaji na kuwaacha wapinzani wao AS Kigali wakitawala Kama wako nyumbani.

Sasa KMC inarejea kwenye Ligi Kuu Bara iliyoanza kesho Jumamosi wakisubiri kuvana na Azam siku ya Jumanne ijayo.
MaoniMaoni Yako