KMC yahapa kuiua AS Kigali kwa Mkapa

KMC yahapa kuiua AS Kigali kwa Mkapa

JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kimataifa dhidi ya AS Kigali utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

KMC inapeperusha Bendera ya Taifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho itacheza mchezo wa marudio dhidi ya AS Kigali Agosti 23 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Rwanda.

Akizungumza na Spoti, Mayanja amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo sawa na wamejipanga kutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo.


“Makosa ambayo tuliyafanya ugenini tumeyafanyia kazi, kwa sasa kikosi kipo tayari kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wetu AS Kigali, mashabiki watupe sapoti.

“Kwa sasa ni wachezaji wachache ambao hawapo fiti ikiwa ni pamoja na Salim Aiyee, Ramadhan Kapela, Charlse Ilanfia, James Msuva na Cliff Buyoya ambaye ameanza mazoezi mepesi,” amesema Mayanja.
MaoniMaoni Yako