Monday, August 12, 2019

KMC leo wachezaji ni mwendo wa bata, KMKM mlima mzito, malindi pia moto

Tags

KMC  leo wachezaji ni mwendo wa bata, KMKM mlima mzito, malindi pia moto
KMC  leo wachezaji ni mwendo wa bata, KMKM mlima mzito, malindi pia moto
JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amewapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake kabla ya kuanza mazoezi kesho kuiwinda AS Kigali hivyo kazi ni kwao kula Bata

KMC ina kibarua cha kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya AS Kigali ya Rwanda.

Sare ya bila kufungana bao italeta matumaini iwapo watashinda mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa kati ya Agosti 23-24.

Wawakilishi wa Zanzibar, KMKM wana kazi kubwa ya kutafuta matokeo mbele ya 1st de Agosto ya Angola baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Amaan kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na itarudiana nao Agosti 24.

Malindi wao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ina kazi ya kutafuta ushindi nyumbani baada ya kulazimisha Sare ya bila kufungana ugenini dhidi ya Mogadishu City ya Somalia.