Monday, August 19, 2019

KMC INA SABABU NNE ZA KUITOA AS KIGALI

Tags1. Ubora wa kikosi
Hili halina ubishi kabisa.. Miongoni mwa timu chache zilizofanya usajili wa maana msimu huu ni KMC.. Imemsajili aliyekuwa mfungaji bora wa Mwadui kwa msimu uliopita, Salim Aiyee.. Ikamsajili aliyekuwa mfungaji bora wa Kagera Sugar, Ramadhani Kapera, wa Ndanda, Vitalis Mayanga na wengine kibao. Imechukua viungo wa nguvu kama Jean Mugiraneza na Kenny Ally.. Kwa kifupi timu imeiva.

2. Uwezo wa Mayanja 
KMC iko chini ya mikono salama ya kocha Mganda, Jackson Mayanja.. Kocha mwenye historia tamu hapa nchini. Mayanja aliwahi kuifanya Kagera Sugar kuwa ya kutisha.. Aliwahi kuifanya Simba kupata matokeo ya kustaajabisha. Hakika akili yake imebeba dhamana kubwa ya mchezo huu. 
3. Sare ugenini
Kwa kupata tu sare ugenini, KMC imethibitisha kuwa ni timu ya ushindani.. Imethibitisha kuwa ni timu bora.. Siyo tu kwamba ilipata sare ugenini, hapana, ilicheza pia kandanda safi. KMC ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga.. Kama KMC ilikuwa bora pale Kigali, itashindwaje kuitoa As Kigali hapa? Haiwezekani.

4. Mipango ya viongozi.
Tayari KMC imekuwa na mipango imara nje ya uwanja.. Viongozi wake wakiongozwa na Meya Sitta wamekuwa imara kimkakati kuhakikisha wanashinda mechi hii.. Kwanza, wamehakikisha wachezaji wako kwenye mazingira mazuri.. Pili wametoa motisha ya kutosha kwa wachezaji wao kuhakikisha kuwa wanajituma zaidi na kupata ushindi.. KWETU MASHABIKI
Kazi yetu mashabiki ni moja tu, kuhakikisha tunakwenda kwa wingi Uwanja wa Taifa Ijumaa hii kuishangilia KMC..Kiingilio ni buku mbili tu... Kumbuka kuwa KMC inafanya jambo la kitaifa. 
KMC tunasema