Saturday, August 17, 2019

Klopp Liverpool amebakiza kazi moja, MOJA TU!

Tags

Klopp Liverpool amebakiza kazi moja, MOJA TU!
Kama ulipata nafasi kuangalia fainali ya UEFA Super cup, katikati ya wiki hii, utakubaliana nami kwamba Kama Liverpool ni mvinyo basi umechachuka vizuri na umefika katika hatua ya kutumiwa na wanywaji wazoefu.
Image result for UEFA SUPER CUP LIVERPOOL 2019
Mabingwa wa UEFA Super Cup 2019, Liverpool
Klabu ya Liverpool kwa zaidi ya muongo mmoja, ilikuwa ikishiriki katika michuano mbalimbali barani Ulaya bila kachukua hata kombe la mbuzi. Katika kipindi chote hicho Liverpool ilipokuwa inatetema, klabu kama Manchester City, Leicester City, Wigan Athletics katika nyakati tofauti zilipanda na kushuka dalaja lakini ziliweza kupata makombe makubwa kama Kombe la Ligi kuu England (EPL), na FA.
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kabla Liverpool hajachukua Kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka huu, Manchester City imechukua makombe 4 ya ligi kuu England na zaidi ya makombe mengine 6 kutoka michuano tofauti, pia, Leicester City ilipanda dalaja na kuchukua kombe la ligi kuu nchini England.
Soccer, Wow, and Hair: LIVERPOOL DID YOU KNOW? ZIDANE HAD HAIR the last time Liverpool won the English league? Wow.
Meme ya Zidane utani kwa Liverpool
Yote yametokea, lakini ni wazi kabisa ukiachana na Manchester United nchini England, Liverpool ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi ya yeyote ile nchini humo. Pia, ukiachana na mafanikio aliyonayo ndani ya England, Liverpool ndiyo klabu yenye makombe mengi sana ya ligi ya mabingwa ulaya (UCL) ukiachana na Real Madrid; binafsi naungana na washabiki wengi wa soka ambao wanasema Liverpool imerudi katika enzi zake huku Jurgen Klopp akiwa ndiye mhandisi mkuu.
https://d3j2s6hdd6a7rg.cloudfront.net/v2/uploads/media/default/0001/89/thumb_88564_default_news_size_5.jpeg
Jumla ya vikombe ilivyoshinda Liverpool mpaka sasa
Jurgen Klopp anarudisha vicheko kwa washabiki wa Liverpool Jurgen Klopp anakuja kama kocha wa kwanza wa kijerumani kufundisha klabu ya Liverpool huku akileta aina tofauti kabisa ya soka. Klopp ametumia zaidi ya paundi milioni 400 kutengeneza kikosi ambacho leo hii kimeleta kombe maarufu zaidi katika uwanja wa Anfield: kombe la ligi ya mabingwa Ulaya.
https://static01.nyt.com/images/2019/06/01/sports/01champions19/01champions19-articleLarge.jpg?quality=75&auto=webp&disable=upscale
Liverpool walipochukua taji la UEFA 2019
Kikosi cha Liverpool kabla ya kuanza kutwaa vikombe hivi sasa, Klopp, alitumia kiasi kikubwa sana cha fedha kununua wachezaji ambao wengi waliamini hawana thamani hiyo na wengine walienda mbali zaidi na kusema Klopp anaifilisi klabu ya Liverpool. Jicho la Klopp liliwaona wachezaji wengi ambao makocha wengi barani Ulaya waliamini hawatakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Liverpool. Wachezaji kama: Virgil Van Dirjik, Mo Salah, Nabi Keita, na Fabinho hawakuangaliwa kama wachezaji watakao kuwa tishio na baadae wachezaji hawa wamekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Liverpool.
Liverpool katika kipindi cha miaka miwili wameshiriki fainali ligi ya mabingwa nakuchukua mara moja, pia katika ligi ya ndani wamekuwa ni washindani wakubwa sana kwa Manchester City ambao hivi sasa ni vigogo wa soka la England, pia wameweza kuchukua kombe la UEFA Super cup kwa kuwafunga Chelsea ambao ni mabingwa wa Uefa Europa league. Najua malengo makuu ya Klopp hivi sasa ni kuhakikisha Liverpool inatwaa kombe la EPL, ndoto ya washabiki wengi wa Liverpool ambao hawajaliona kombe hili kwa zaidi ya miaka 28, je, Klopp atafanikisha?
Image result for LIVERPOOL epl 1991
Liverpool walipochukua ubingwa wa EPL, msimu wa 19989-90
Ndiyo Klopp anakwenda kuwapa Liverpool kombe la EPL
Washabiki wengi wa soka wana amini katika bahati lakini wengi hawakubali kuwa soka ni mipango, uwekezaji pamoja na muda (timing), leo hii Klopp anakuja katika timu ambayo asilimia zaidi ya 90 hawajawahi kuwa na uzoefu wa kutwaa makombe lakini Klopp ameweza kuwabadilisha wachezaji kama Andy Robertson, Joseph Gomez, Alexander-Arnod, Virgil Van Dijk, Sadio Mane, Mo Salah, Jordan Henderson, Georginio Wijnaldum Divoki Origi na wengine kuwa katika mentality ya mabingwa na wamefanikiwa kufika katika level ambayo Klopp alitaka.

Pia, wengi wanahoji mmetoka nini Pep Guardiola achuke makombe mawili ya EPL mfululizo katika kipindi kifupi tangu aje England? ni wazi kabisa Pep amekuja katika klabu ya Man City na kuwakuta wachezaji kama David Silva, Toure Yaya, Vincent Kompany, Sergio Aguero, Fernandinho ambao wanauwezo pamoja na uzoefu wakiushindani tofauti na Klopp.
https://miro.medium.com/max/1200/0*_d6p-ce5nd_FOJOG
Kocha wa Man City, Pep Guardiola ambaye ni mpinzani mkubwa wa Klopp EPL
Klopp amesajili na kupandisha vijana wadogo ambao hawana uzoefu na ameweza kuwafanya hatari duniani. Nani anapinga hivi sasa kuwa Van Dirgik ni beki bora zaidi duniani? pia hakuna ubishi kwamba Liverpool ndiyo kikosi ambacho kina wachezaji wanaohitajika na klabu nyingi duniani. Wachezaji kama Salah, Van Dirgik, Mane, Robertson, Allison Beker, Fabinho, Keita ni mfano mdogo ambao haupingiki.
Image result for VAN DIJK LIVERPOOL
Nahodha wa Liverpool, Van Dijk
Ndiyo maana nilipoanza nikasema kama Liverpool ni mvinyo, basi huu mvinyo umechachuka na umefika hatua ukipiga fundo moja tu, unalewa. Klopp yupo katika vita, vita hii mwaka huu basi itakuwa si mchezo; mwaka uliopita kutokana na uzoefu mdogo katika ligi, Liverpool waliwapa Man City ubingwa dakika ya mwisho. Naamini Klopp pamoja na kikosi chake wamejifunza mengi kutoka kwenye msimu uliopita basi mwaka huu patakuwa hapatoshi.
Image result for liverpool
Jurgen Klopp na vijana wake wakisherehekea ubingwa wa UEFA Super Cup
Upana wa kikosi, umahiri wa wachezaji, ushabiki wa damu pamoja na weledi wa kocha ni kitu pekee ambacho ukiwa kama mshabiki wa soka huwezi pinga kuwa Liverpool wanaingia katika msimu wa 2019/20 wakiangalia kombe la EPL kama uhai wao.