Kagere ni bonge la mfungaji - GADIEL MICHAEL

Kagere ni bonge la mfungaji - GADIEL MICHAEL

Beki mpya wa Simba Gadiel Michael amesema mshambuliaji Meddie Kagere ni mchezaji matata aliyewahi kukumbana nae

Gadiel aliyetua Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Yanga, amesema Kagere ni aina ya mshambuliaji ambaye beki yeyote hatapenda kukutana nae

Juzi kwenye mazoezi ya Simba viwanja vya Gymkhana, Gadiel alionja 'joto ya jiwe' baada ya kupangwa kumkaba Kagere

Katika mazoezi hayo, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, aliwapanga wachezaji wawili wawili, mshambuliaji na beki kuchuana katika kujenga stamina na kuwapa mbinu za kukaba na kushambulia.

Kila kundi lilianza na zoezi la viungo kusaka pumzi kabla ya kumalizia katika kucheza na mpira, beki akitakiwa kumdhibiti mshambuliaji asipenye, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha safu ya ulinzi, lakini pia kuwaongezea makali washambuliaji.

Baada ya kuonyeshana kazi katika zoezi la kusaka pumzi, lilipokuja lile la kuchezea mpira, Kagere alimtesa mno Gadiel kwa kumchezea kadri alivyotaka na kumpita kirahisi na kumwacha akidondoka akiwa hoi na beki huyo kuishia kucheka akionekana kuukubali 'muziki' wa straika wao huyo.

"Kagere ni miongoni mwa washambuliaji ninaowakubali sana hapa Tanzania. Nimekuwa nikitamani kufahamu siri ya mafanikio yake kwani ni mchezaji ambaye yuko fit sana," amesema

"Kumkaba ni changamoto, lakini kikubwa nafurahi nacheza nae timu moja na nitaweza kujifunza mengi zaidi kutoka kwake"
MaoniMaoni Yako