KAGERA SUGAR: Makosa yetu mwisho ni msimu uliopita

KAGERA SUGAR: Makosa yetu mwisho ni msimu uliopita
KAGERA SUGAR: Makosa yetu mwisho ni msimu uliopita

UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa kwa sasa umejipanga vema kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2019/20 unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Meky Maxime amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani msimu ujao na kinatarajia kufanya kweli kwa timu zote watakazokutana nazo.


Msimu uliopita wa mwaka 2018/19 Kagera Sugar ilijikombea pointi sita mbele ya Simba na ilikuwa kwenye hatihati ya kushuka daraja ikapeta kwenye mchezo wa playoff mbele ya Pamba FC kwa ushindi wa mabao 2-0.


“Tumefanya usajili makini na kwa kuzingatia mahitaji yetu ni dalili tosha kwamba tupo tayari kwa ushindani ndani ya ligi, hatutafanya makosa kama msimu uliopita wapinzani wetu wajipange.


“Maandalizi yetu si kwa ajili ya Biashara United pekee, ni kwa timu zote ambazo tutakutana nazo ambazo ni pamoja na Simba, Yanga, Azam FC mpaka Lipuli tutafanya kweli,” amesema Maxime.


Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Kagera Sugar ni pamoja na Benedict Tinocco,Hassan Isihaka, Awesu Awesu na Everist Mujwahuki.


Mchezo wa kwanza kwa Kagera Sugar utakuwa dhidi ya Biashara United utakaochezwa Uwanja wa Karume, Mara.
MaoniMaoni Yako