Monday, August 12, 2019

Juma Abdul, Andrew Vincent pasua kichwa Yanga, Tamko la uongozi hili hapa

Tags

Juma Abdul, Andrew Vincent pasua kichwa Yanga, Tamko la uongozi hili hapa
FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa bado hajajua wachezaji wa Yanga ambao hawajajiunga na kikosi watarejea lini kwa sasa.

Juma Abdul na Andrew Vincent 'Dante' hawakujiunga na kikosi kambini Morogoro hata timu ilipojichimbia Visiwani Zanzibar hawakugusa kambini kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa wanadai stahiki zao.

Habari zinaeleza kuwa beki kisiki, Kelvin Yodani yeye amejiunga na timu ila sharti lake ni moja kama ilivyo wa wenzake kwamba ni lazima alipwe stahiki zake zote.

Mwakalebela amesema kuwa:"Kwa sasa sijajua wachezaji hao watarejea lini kambini kwa kuwa wao ndio walianza kugoma,

"Ni wachezaji muhimu na mchango wao ni mkubwa kama ambavyo walipambana msimu uliopita ila kwa sasa uongozi tutakaa ili kumaliza matatizo haya," amesema.