Monday, August 12, 2019

Hamisa mobeto leo kupiga live na bendi yake Dar live, awaita mashabiki

Tags

Hamisa mobeto leo kupiga live na bendi yake Dar live, awaita mashabiki
HAMISA Mobeto, mwanamitindo na mwanamuziki amewaambia mashabiki wake kujitokeza kwa wingi leo Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem kupata burudani kutoka kwake.

Mobeto amesema: “Kikubwa watu watarajie burudani kali kutoka kwangu, watu waje kwa wingi niwape burudani bila kikomo.

“Najua wengi wana hamu ya kumuona Mobeto, hivyo fursa ndiyo hii na siyo ya kukosa kabisa kwani kwa mara ya kwanza nitaimba nyimbo zangu live kwa kutumia bendi kuanzia wimbo wa Sawa, My Love, Tunapendana na nyingine nyingi,” amesema Mobeto.

Katika tamasha hilo kiingilio kitakuwa ni Sh 5,000 tu, wasanii wengine watakaokuwepo ni Mr. Blue, Chidi Benz, Mzee wa Bwax na Easy Man.