HAJI MANARA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI LEO.. KUHUSU NAFASI YA USEMAJI KATIKA KLABU YA SIMBA.


Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ametangaza viingilio vya mchezo wa jumapili wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ud Songo ya Msumbuji. Manara amesema hawezi kukaa katika kiti hicho milele na kwamba itafika siku ataondoka na mwingine atakikalia. Hata hivyo amewataka mashabiki wa soka watambue hadi sasa @hajismanara ndiye Msemaji wa klabu hiyo hadi hapo itakapotangazwa tofauti.

Haji ambaye amekiri hakuna tatizo klabuni hapo alikuwa akijibu swali la Mwanahabari aliyetaka kufahamu juu ya hatma yake kufuatia taarifa zinazosema @giftmacha_official amemalizana na vigogo hao ili awe mrithi wa msemaji huyo anayesifika kwa hamasa.


"Kwetu mashabiki sio mchezaji wa 12, ni mchezaji wa kila nafasi uwanjani. Tunashinda lakini mashabiki wanachangia sana"

 "Simba ndio timu ambayo imeongoza msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa  Haji Manara. #NguvuMoja

 "Na bahati nzuri mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa umepangwa siku nzuri. Utakuwa Jumapili saa 10 jioni."-

 "Tunataka mashabiki mshabikie mwanzo mwisho. Tusisubiri mpaka Shiboub apige mtu chenga, mashabiki tunaenda uwanjani kushabikia."-

 "UD Songo sio timu ya kupeza. Tumeona mechi yao wamecheza vizuri. Nawaomba mashabiki wa Simba siku hiyo tujitokeze kwa wingi."-
 "Kwa mashabiki wa Simba hii ni Champions League, kazi yetu mashabiki ni kushabikia, twendeni."
 "Matumaini yangu tutawatoa UD Songo. Kwa maandalizi yetu, mipango na mapenzi ya Mungu tutashinda."

 VIINGILIO VYA JUMAPILI TAIFA
5,000/=, 15,000/=, 30,000/=
Platinum 100,000/=
Platinum plus 150,000/=
UD Songo watawasili Ijumaa.
MaoniMaoni Yako