Wednesday, August 7, 2019

Familia yamrudisha Rooney England

Tags

Familia yamrudisha Rooney England
London, England. Wayne Rooney amesema familia ndio imemuondoa DC United na kujiunga na Derby County.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United, alisema familia ni jambo muhimu, hivyo hakuwa na sababu ya kupinagana nayo.

Rooney alisema alizugumza na mkewe Coleen kuhusu shule ya watoto wao wannne kabla ya kufikia mwafaka.

Nahodha huyo wa zamani wa England, anatarajiwa kujiuanga na Derby akiwa mchezaji na kocha Januari, mwakani baada ya kutia saini mkataba wa miezi 18.

Rooney alitoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza namna alivyofanya uamuzi wa kushitukiza wa kujiunga na Derby.

Alisema siku zote amekuwa akitoa kipaumbele kwa familia yake, hivyo alipopata ofa ya kwenda Derby alijadiliana na mkewe kabla ya kuchukua uamuzi.