Wednesday, August 7, 2019

Everton yapeleka Pauni 100 mil kwa Zaha

Tags


Everton wamekusanya kiasi cha Pauni 100 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, 26. Ofa hiyo inahusisha pia Everton kuwapa Palace mshambuliajii Cenk Tosun na kiungo James McCarthy, wote wana miaka 28. Wachezaji hao wawili watakaokuwa sehemu ya dili hilo wana thamani ya Pauni 35 milioni, hivyo kulifanya dili zima la kumnyakua Zaha kufikia Pauni 100 milioni.

Kabla ya Everton kujitokeza kwa nguvu katika dili la kusaka saini ya nyota huyo, Manchester United walikuwa wakimtaka kwa nguvu hadi pale dau lao la Pauni 55 milioni lilipogomewa na Palace iliyosisitiza kulipwa Pauni 65 milioni.

Zaha, nyota wa zamani wa United na Chelsea, ana kipengele katika mkataba wake wa kurejea Crystal Palace kinachoibana klabu hiyo kumuuza Man kwanza, lakini iwapo itashindikana basi asilimia 20 ya mauzo yake kokote atakakouzwa yataingia kwenye fuko la mabingwa hao wa zamani wa England.