Daktari Yanga Awatoa Hofu Mashabiki Kuelekea Mchezo Dhidi Ya Township Rollers


Daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema kuwa mpaka sasa wachezaji wote 20 wspo vizuri licha ya changamoto ya uchovu wa safari waliokua nao baadhi ya wachezaji.

Aidha ameongeza kua nahodha wa wanakijani na manjano hao, Papy Tshishimbi aliyekua akisumbuliwa na Mafua sasa yuko timamu  wawe tayari kwa mchezo.

. "Tumekuja na wachezaji 20 ni kweli kwamba kulikuwa na shida kidogo safari ni ndefu na mnajua tulipotoka na tumeanzia Arusha
Na kupaa na moja kwa moja mpaka Nairobi
.
.
Nairobi moja kwa moja mpaka South Afrika,
halafu tulitumia masaa 6 kutoka Johannesburg kuja mpaka Gaboroni, Botswana .
.
Kuna baadhi ya wachezaji walikuwa na uchovu kidogo lakini tangu juzi, jana mpaka leo hii nashukuru kwamba wote wapo salama
Isipokuwa tu Jana kuna mchezaji mmoja Papy Tshishimbi Kabamba, alikuwa na matatizo kidogo ya mafua, lakini baada ya matibabu leo yuko salama .
.

Kwaiyo labda niwaambie tu wana-Yanga na Watanzania kwaujumla kwamba timu sasa iko safi na bahati nzuri hakuna mchezaji ambaye anamajeraha mpaka sasa .
.

Labda nilikuwa nafikiri kwamba kutakuwa na hali ya hewa kidogo ya ubaridi lakini kumbe hali ya hewa iliopo hapa sasa ni sawa tu na Dar es salaam, mi sioni tofauti .
.

Kwaiyo pamoja na kwamba tulikaa Arusha kwenye hali ya hewa ambayo ni baridi sana lakini kwasasa wachezaji mpaka sasa wameshazoea
Kwaiyo katika hilo sioni kama kunatatizo lolote mpaka sasa

MaoniMaoni Yako