Wednesday, August 7, 2019

Coutinho aziingiza vitani Arsenal, Spurs

Tags

Klabu ya Arsenal imejipanga kunasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Philippe Coutinho kwa mkopo.

Kiungo huyo alianza safari iliyochukua takribani saa 10 kwenda Florida, huku jina la Mbrazili huyo likitawala kwenye vyombo vya habari vya kijamii kuhusu uhamisho huo.

Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Hispania El Larguero, mpango wa Arsenal kwa mshambuliaji "umefungwa kabisa."

Timu mbili zinazojulikana kumwania nyota huyo wa zamani wa Liverpool kwa mkopo kutoka Nou Camp, ni Arsenal pamoja na Tottenham.

Lakini muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili England unaelekea ukingoni, hivyo atalazimika kurudi haraka Ulaya ili kukamilisha uhamisho wake.

Inaaminika Arsenal iliongoza matamanio kwa Coutinho baada ya kukutana na viongozi wa Barca wakati wa mchezo wa Kombe la Gamper uliofanyika Jumapili iliyopita.