Tuesday, August 13, 2019

Benitez: Kukosa uaminifu sababu ya kuondoka Newcastle

Tags

Benitez: Kukosa uaminifu sababu ya kuondoka Newcastle
Kocha Rafael Benitez amedai kuwa kukosekana kwa ‘uaminifu’ kwa sababu ya ‘ahadi zisizotekeleza kwa miaka mitatu’ kutoka kwa bodi ya Newcastle ndiyo sababu ya kuachana na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Benitez amejiunga na timu Dalian Yifang inayoshiriki Ligi Kuu China ‘Chinese Super League’ baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Newcastle mwishoni mwa Juni, bajeti ndogo iliyowekwa na mmiliki Mike Ashley ndiyo sababu ya timu hiyo kumaliza ligi katika nafasi ya 13 msimu uliopita.

Akijibu madai yaliyotolewa na mkurugenzi wa Newcastle Lee Charnley mwishoni mwa wiki kwamba Benitez aliondoka "kwa sababu pesa", Mhispania alisema kama hiyo ndiyo sababu "basi angeweza kufanya uamuzi huo mapema zaidi".

"Bodi ya Newcastle ilikuwa na mwaka mzima wa kujadili mkataba wangu, lakini tulipokutana mwisho wa msimu uliopita, walishindwa kunipa dau lililolita," Benitez alisema katika kolamu yake The Athletic.

"Waliniambia hawataki kuwekeza katika uwanja wa michezo au uwanja wa mafunzo - ikiwa wanapenda, naweza kuelezea sababu iliyomfanya Mike Ashley kukataa kufanya hivyo. Maoni yao ya mradi ilikuwa sera ya kusaini wachezaji chini ya miaka 24, kwa maoni yangu, bajeti inayopatikana haitoshi kushindana kwa 10 bora.