Saturday, August 17, 2019

Baada Ya Kusakamwa Sana, Dismas Ten Akutana Na Haji Manara, Azungumza Mazito

Tags

Baada Ya Kusakamwa Sana, Dismas Ten Akutana Na Haji Manara, Azungumza Mazito


Sikia nikwambie brother..! Watu wengi sana ambao huwa WANAFURAHIA ANGUKO la WENZAO ama wanatamani KUFELI kwa WENGINE huwa wanakuja kukutana na ANGUKO LA AIBU kwenye maisha yao.
.
Unakuta mtu anapanga njama kumfanya mtu mwingine achukiwe na bosi wake.Unakuta mtu anaweka mpango wa siri ili kukatisha NDOTO ZAKO, kuna watu wanathubutu hata kupanga mbinu ya KUMWANGUSHA au KUMCHAFUA mwingine wakiamini hiyo itawasaidia,lakini mwisho wake wanagundua aibu inawakaribia.
.
Moja ya Kitu ambacho unatakiwa kujifunza kwenye maisha ni KUFURAHIA MAFANIKIO YA WENGINE,KUSHEHEREKEA KUINULIWA KWA WENGINE na KUTAMANI KUNG’ARA KWA WENGINE.
.
Kwa taarifa yako HAKUNA mwenye UWEZO wa KUCHUKUA nafasi YA mwingine,(kuwa kama yule) anaweza kujaribu kwa MUDA mfupi tu lakini kuna kitu kitatokea na ATAIPOTEZA.Kama vile ambavyo Kila NYOTA INA SEHEMU YAKE MAWINGUNI na kila mmoja inang’aa kwa NAMNA yake, vilevile kila mtu ni “STAR” kwa namna yake, Waombee wengine mema na mafanikio, MUNGU atakurudishia MARADUFU.
.
Nakuombea MUNGU aendelee kukufanikisha KINYUME na wanaotamani ANGUKO LAKO.
.
USIHANGAIKE KUZIBA NYOTA ZA WENGINE ZISIN’GAE,HANGAIKA KUIFANYA YA KWAKO ING’AE ZAIDI.

Na Dismas Ten