Azam FC yasahau maumivu ya kupoteza ngao ya jamii, sasa ni mwendo wa kimataifa

Azam FC yasahau maumivu ya kupoteza ngao ya jamii, sasa ni mwendo wa kimataifa


UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa unasahau habari za kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba uliochezwa Jumamosi sasa nguvu kazi ni kwenye mchezo wa kimataifa.

Azam FC lipoteza kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Simba mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Taifa sasa wameanza maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Fasil Kenema.

Mchezo huo wa marudio utachezwa Uwanja wa Chamazi majira ya saa 10:00.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu ila wamejipanga kupata matokeo chanya.

Mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Ethiopia Azam FC ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 kazi kubwa Jumamosi ni kupata ushindi ili kusonga mbele.
MaoniMaoni Yako