Al Ahly fc Wavunja Rekodi Ya Yanga CAF Champions League Iliyowekwa Miaka 10 IliyopitaMashetani wwekundu wa jiji la Cairo nchini Misiri hapo jana wameibuka na ushindi mnono wa goli 9-0 dhidi ya Atlabara FC ya Sudani Ya Kusini na kuivunja rekodi ya Yanga ya Tanzania iliyowekwa miaka 10 iliyopita.

Baada ya ushindi huo sasa Al ahly inafuzu hatua inayofuata kwa Agrigate ya 13-0 na hii ni baada ya ushindi wa awali wa goli 4-0 ilioupata kwatika mchezo wa kwanza.

Ikumbukwe Yanga mnamo mwaka 2009 iliweka rekodi ya kuibuka na ushindi mnono katika mechi za raundi ya kwanza CAF Champions League wa jumla ya goli 8-1 dhidi ya Etoile d'Or ya Comoros mchezo uliopigwa kwenye dimba la taifa na kukamilisha mchezo wa pili kwa kuibugiza kipigo cha goli 6-0 mchezo uliopigwa huko Comoros....

Kwa faida ya wasomaji katika ushindi huo wa goli 8-1 wafimgaji ni:-
Young Africans 8 – 1 Etoile d'Or

Boniface Ambani 2' 71' (pen.) 80' 85' Abubakar Alisouf 20'
Jerry Tegete 53' 76'
Wisdom Ndlovu 74'
Mrisho Ngassa 81'
MaoniMaoni Yako