AJIBU AREJEA MZIGONI SIMBAMshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajibu ameanza mazoezi mepesi baada ya kuanza kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua.

Ajibu alipata majeraha akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichokuwa kinajiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Kenya.

Katika mazoezi ya mabingwa hao yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana leo asubuhi Ajibu alionekana akiwa na kocha wa viungo Adel Zrane akipewa mazoezi binafsi.

Simba inajiandaa na mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya UD Songo ambao utafanyika katika uwanja wa Taifa siku ya Jumapili saa 10 jioni.
MaoniMaoni Yako