Yanga waanza kuitisha Biashara


Akizungumza na gazeti hili jana, Zahera alisema hajafurahishwa na matokeo ya michezo yao miwili iliyopita dhidi ya Stand United na Kariobang Sharks) ambayo walipoteza, amepania kuirejesha timu yake katika matokeo ya ushindi.
Zahera alisema kuwa kama wataruhusu kupoteza mchezo huo dhidi ya Biashara watajiweka katika wakati mgumu na morali ya wachezaji itashuka huku wakijiweka kwenye nafasi ngumu ya kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa.
“FA ni michuano mikubwa ambayo inatoa mwakilishi wa nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, malengo yetu ni kuchukua kombe hil, tunaendelea kujipanga ili tufikie mipango yetu,” alisema.
Wakati huo huo, habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuanza kupona kwa wachezaji wake waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Wakati viungo Papy Thshishimbi na Thaban Kamusoko ambao walikuwa majeruhi wameanza kucheza katika mchezo wa michuano ya Sportpesa dhidi ya Kariobang Sharks Jumanne iliyopita, kiungo mwingine wa timu hiyo, Raphael Daudi naye ameanza kujifua.
Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, aliiambia gazeti hili kuwa Daudi ameanza mazoezi mepesi na amepewa programu maalum ambayo itamweka fiti na hatimaye kurejea uwanjani kuitumikia klabu yake.


“Kupona kwa wachezaji waliokuwa majeruhi ni jambo jema kwa sababu kunatoa wigo mpana kwa kocha (Zahera) kupanga kikosi chake kwa uhuru, Raphael ameanza mazoezi na anaendelea vizuri,” alisema Saleh.
Yanga inahitaji kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la FA au kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika hapo mwakani.
MaoniMaoni Yako