Yanga Kupewa Pointi Tatu Mezani Kutoka Klabu ya Stand United Baada Ya Kukata Rufaa

Yanga  Kupewa Pointi Tatu Mezani Kutoka Klabu ya Stand United Baada Ya Kukata Rufaa
YANGA ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stand United, lakini mechi hiyo imeanza kuibua zengwe baada ya kiungo mmoja kudaiwa kufanya udanganyifu.
Iko hivi, Stand United katika mchezo huo walikuwa na kiungo mmoja fundi, Afidh Mussa pale kati mwenye leseni namba 000238M93 ya kucheza Ligi Kuu Bara.
Lakini, taarifa zinadai kuwa kiungo huyo hakuwa halali kucheza kama mchezaji mzawa baada ya kuwahi kubadili uraia wake.
Inadaiwa Mussa aliwahi kuondoka nchini kwenda kucheza soka Burundi, ambapo huko alibadili uraia na kupata nafasi ya kuichezea timu ya Taifa ya Burundi akiwa amebadilisha mpaka jina.
Akiwa Burundi Afidh alikuwa akitambulika kama, Hererimana Hafidh na kucheza timu ya taifa ya wakubwa.
Yanga yamkatia
Yanga baada ya kusikia taarifa hizo wakawahi kukata rufaa wakipinga uhalali wa kiungo huyo kuichezea Stand United wakitaka kuona Bodi ya Ligi itoe maamuzi juu ya kiungo huyo na klabu yake.
“Tumemkatia rufaa, tumeshaiandaa nafikiri itawasilishwa haraka leo (jana mchana) au kesho (leo) huyu sio mchezaji halali tumejiridhisha,” alisema mmoja wa mabosi wa Yanga.
Afidh huyu hapa
Baada ya kuibukla kwa sakata hilo Mwanaspoti lilimtafuta Afidh, ambaye alikiri kucheza soka nchini Burundi kisha kuja nchini. Kiungo huyo alikiri kuichezea timu ya Taifa ya Vijana ya Burundi, lakini akakanusha kucheza kikosi cha wakubwa.
Pia, alisema amewahi kuichezea Vitalo (Burundi), Police FC (Rwanda), Lupopo FC kisha DC Motema Pembe zote za DR Congo na kusisitiza, yeye ni Mtanzania halisi.
Hadi Tambwe kamtambua
Wakati Mwanaspoti linatafuta uhalali huo lilimtafuta mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ambaye alikiri kumtambua Afidh akisema aliwahi kucheza naye timu ya Taifa ya Intamba M’urugamba
“Namjua Afidh kwani hapa ni Mtanzania? Nakumbuka nilicheza naye timu ya taifa ya wakubwa kule nyumbani ingawa sijui sasa hapa anachezaje, hayo mumuulize mwenyewe,” alithibitisha Tambwe.
Zahera afunguka
Kocha Zahera alifunguka jana kuwa anamjua vyema kiungo huyo na kama atacheza kama Mtanzania nchini hilo linaweza kuwa kosa kubwa.
“Kosa kama hili kule kwetu Kongo timu hiyo iliyofanya hivyo inapokonywa pointi ambazo mchezaji husika alicheza na mchezaji pia anafungiwa na nakumbuka huyu alicheza mpaka Kongo nitauliza huko ili kuona jambo hilo limekaaje.”
MaoniMaoni Yako