Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali

Mabadiliko yamejiri baada ya kipindi cha muda mrefu lakini pia ni mchakato wa polepole.
Tabia nyingine zinazidi kusalia katika vizazi vingi hata baada ya kukosa madhumuni.
Vipengele hivi vya uvumbuzi, au sifa za kimwili, hupatikana katika wanadamu pia.
"Mwili wako kimsingi ni makumbusho ya historia ya asili," anasema mwanahistoria wa binadamu Dorsa Amir katika chapisho lake la mtandao wa Twitter.
Kwa nini sifa hizi zinaendelea kusalia hata ingawa zinaonekana kupoteza umuhimu wao? Kwa sababu mabadiliko ni mchakato wa taratibu.
Wakati mwingine, hakuna shinikizo za kutosha dhidi yake, kwa hiyo inasalia kutoka kizazi kimoja hadi chengine.
Katika baadhi ya matukio, hupata kazi mpya katika mchakato wakati vinapofanya kazi mpya.
''Mara nyengine unafikiri labda, je viungo hivi vilitakiwa kutoa huduma gani'', Dorsa Amir aliambia BBC.
Hivi hapa ni viungo hivo sita vilivyowachwa.
1. Mmisuli iliopo chini ya kiganja cha mkono
Kwa mfano weka mkono wako katika eneo lililo tambarare kama meza halafu uguse kidole kidogo hadi kile kikubwa cha mkono wako.
Je unaona misuli karibu na kiganja chako cha mkono ? hiyo ndio inayoitwa Palmaris longus.
Usijali kama huwezi kuona. Takriban asilimia 18 ya watu duniani hawana misuli hiyo na kutokuwepo kwake hakushirikishwi na mapungufu yoyote.
Misuli hiyo hupatikana miongoni mwa sokwe wanaopendelea kupanda miti.
Hii inamaniisha kwamba ilikuwa ikitumika kusaidia kupanda miti.
Siku za hivi karibuni misuli hiyo hupendelewa sana na madaktari wa upasuaji.
''Huitumia mara kwa mara katika upasuaji kwa kuwa haitumiki sana katika kazi za mkono'', alisema Dorsa.
2. Uvimbe mdogo katika sikio.
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
"Iwapo unaweza kuchezesha sikio lako basi unaonyesha mabadiliko ya binadamu'', anaandika Jerry Coyne katika kitabu chake.
Kwa ni mabadiliko ni ya kweli.
Alikuwa akizungumzia misuli mitatu iliopo nje ya sikio. Uvimbe mdogo uliopo juu ya sikio ni mojawapo ya misuli hiyo.
Miongoni mwa watu wengi, misuli hiyo haina maana yoyote lakini wanaweza kuitumia kuchezesha masikio yao.
Huku ikiwa kuna mjadala wa iwapo msuli huo ulikuwa mkubwa miaka ya mbeleni, inadaiwa kuwa msuli huo katika sikio unaonyesha mabadiliko.
Misuli hiyo hutumika miongoni mwa paka na farasi kuchezesha masikio yao kama inavyoelezwa na Coyne.
Inawasaidia kukabiliana na wanyama wengine, kuwatafuta watoto wao na kuelewa sauti nyengine.
3. Mfupa wa mkia
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
Mfupa wa mkia bila shaka ni mabaki ya mabadiliko katika binadadamu, kulingana na Dorsa Amir.
Inatukumbusha kwamba tulikuwa na mikia ambayo litumika kusawazisha mwendo wetu katika miti.
Kiungo hicho ni mojawapo ya mifano mizuri ya viungo vinavyofanya kazi nyengine kinyume na ilivyokuwa awali.

4. Kigubiko cha jicho la tatu
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
Je unaiona sehemu ya rangi ya waridi iliopo katika kona ya jicho lako?
Ni mabaki ya kile kinachojulikana kama utando au "kigubiko cha tatu", kutokana na mabadiliko ya mwanadamu.
Kigubiko cha jicho la tatu husonga kutoka kushoto kwenda kulia, kulingana na Dorsa.
Lakini kwa sasa hakina huduma yoyote katika maisha ya sasa.
Unaweza kukiona miongoni mwa wanyama wengine , kama vile ndege na paka.
5. Msisimko wa mwili bila kutarajia
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
Je unajua kitendo anachofanya paka wakati anapohatarishiwa maisha yake?
Ni sawa na vile tunavyopata msisimuko wa mwili wakati unaposikia baridi ama hata kuogopa kitu.
Wanasayansi wanakiita kitendo hicho piloerection reflex
Kutokana na vile tunatumia muda wetu mrefu duniani kama wanyama wenye manyoya, msisimuko huo ulikuwa ni mojawapo ya njia za zamani za kukufanya uwe mkubwa zaidi ya ulivyo ama hata kulinda joto kutotoka mwilini wakati unapohisi baridi kulinga na Dorsa
''Wakati tulipoanza kupoteza baadhi ya nywele hizo mwilini , msisimuko huo ulianza kukosa maana hadi kufikia kiwango cha kukosa kazi ya kufanya''.

6. Mshikamano wa mikono

Mshikamano wa mkono unaonekana wakati mtoto anaposhikilia kidole kwa nguvu.
Kitendo hiki hufanyika miongoni mwa wanyama wengine.
''Watoto huzaliwa tayari kuwashika wazazi wao ili kubebwa, inadaiwa kwamba kitendo hicho miongoni mwa wanadamu kilitokana na kitendo hicho'', anaongezea Dorsa.
Lakini watoto wetu hubebwa wakiwa hawajakomaa vya kutosha ikilinganishwa na watoto wa wanyama wengine ambapo hawawezi kuinua vichwa vyao na kutembea.
Hizi ni tabia nyengine ambazo zinatokana na mabadiliko ya mwanadamu. lakini ni mabadiliko ambayo hayamsaidi mwanadamu wa sasa.
MaoniMaoni Yako