‘Uchebe’ kupima mashine 3 SportPesa

‘Uchebe’ kupima mashine 3 SportPesa

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema wachezaji watatu wanaofanya majaribio kwenye kikosi chake wataanza kutumika leo kwenye mashindano ya SportPesa ili kutoa nafasi kwa benchi la ufundi kujiridgisha juu ya uwezo wao kabla ya kuwasajili.
“Unajua kwamba kwenye kombe la SportPesa tunaruhusu kujaribu wachezaji na sisi tumeamua kufanya hivyo kwa kuleta wachezaji watatu ambao tutakuwanao kwa wiki moja wawili tuko nao na mmoja atafika leo (jana).”
“Kikubwa ni kuangalia namna tutakavyoweza kufanya usajili wa wachezaji hao ambapo mmoja ni beki na wawili ni washambuliaji.”
“Ukiangalia mechi yetu dhidi ya AS Vita, moja ya sehemu zilizokuwa na mapungufu ni eneo la beki. Siku 7 zinatosha kupima uwezo wa mchezaji na wachezaji hawa watacheza mechi zote tatu za SportPesa ili tujiridhishe kuhusu uwezo wao.”
“Ni kweli huu unaweza kuwa usajili wetu wa CAF hatua hii ya makundi kama utaenda vizuri na lazima tuchague kati yao kulingana na viwango vyao lazima tufanye maamuzi ili kwenda sawa na kanuni ya ligi kuu ya wachezaji 10.”
“Tuna Juuko, Wawa na Nyoni ambaye ni majeruhi, kwenye nafasi hii kama mmoja ataumia unaona namna ambavyo tutakuwa kwenye matatizo hivyo kuona hilo nalo.”
“Kuhusu kombe la SportPesa ni zuri lakini halina tofauti sana na kombe la Mapinduzi nina wachezaji 22 ambao ni wazima hivyo nitawapa nafasi zaidi wale ambao hawakucheza Mapinduzi.”
“Kiukweli kombe hili sio target yangu ila nafahamu ni muhimu kwa sababu SportPesa ni wadhamini wetu japo najua bingwa atacheza na Everton, inaweza kuwa nzuri kwa wachezaji wetu kukutana na timu kama hiyo yenye wachezaji wenye viwango vikubwa.”
“Lakini sio mpango wangu, maandalizi yangu kwa sasa ni dhidi ya mchezo wa Misri dhidi ya Al Ahly lakini wakati huo tuna mechi 24 za ligi kuu za kucheza ndani ya miezi mitatu.”
“Kwa ratiba higo kazi itakuwa kucheza kupumzika, kusafiri na kucheza na ambapo tunaweza kuona namna ambavyo hatua ya ligi ya kawaida. Ni kweli kwamba TFF inapaswa kuzipanga mechi zote hizi na kuhakikisha zinachezwa, ni ngumu kwetu kwa sababu ukiangalia tayari kuna timu zina mechi 23 na sisi tuna mechi 14.”
“Kwa sasa baadhi ya wachezaji wetu ni majeruhi kama Asante Kwasi, Kapombe, Nyoni na Salamba, Bocco na Mlipili.”