Thierry Henry asimamishwa kazi AS Monaco

Thierry Henry asimamishwa kazi AS Monaco

Kocha Mkuu wa AS Monaco, Thierry Henry amefukuzwa kutokana na timu hiyo kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya.

Taarifa hiyo ya kusimamishwa imekuja siku mbili baada ya kutolewa katika French Cup na Metz. klabu inasema kuwa, wamesimamisha kazi Thierry Henry wakati wakiwa wanasubiri maamuzi ya mwisho kuhusu mustakabali wake.

Timu hiyo haijashinda mchezo wowote wa ligi tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana walipoifunga Amiens bao 2-0.

Henry ameichukua Monaco miezi mitatu iliyopita na tangu achukue kazi hiyo timu hiyo imezidi kufanya vibaya.
MaoniMaoni Yako