Simba yajipanga kuitesa Bandari


Simba, wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki na Kati waliobakia katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefika hatua hiyo baada ya kuwafunga Wakenya, AFC Leopards mabao 2-1 wakati Bandari iliwaondoa Singida United kwa kuwachapa goli 1-0.
Kocha wa makipa wa Simba, Mwarami Mohamed, alisema jana kuwa, timu yao imejipanga kuendelea kuipa heshima Tanzania kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo na hatimaye kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza ikiwa na kikosi kamili.
Mwarami alisema kuwa, wamejiandaa kukutana na ushindani katika mechi hiyo na vile vile wanawaheshimu wapinzani wao, Bandari ambao wanafundishwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Ben Mwalala.
"Tunaangalia nini tunataka kufanya, kuhusu kikosi chetu yoyote anaweza kucheza, anaweza hata akaanza Ally (Salim), Dida (Deogratius Munishi), hiyo tutajua hapo kesho (leo)," alisema kipa huyo wa zamani wa Timu ya Tanzania (Taifa Stars).
Mwalala alisema kuwa Simba isitarajie mteremko katika mechi ya leo na tayari wameshawaangalia namna wanavyocheza.
"Tunajua wapi wana nguvu na wapi wana matatizo, naamini tutaingia kwa ajili ya kusaka ushindi na hatimaye kucheza fainali," alisema Mwalala ambaye alitamani zaidi kukutana na timu yake ya zamani.
LAMINE KIMEELEWEKA
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa mshambuliaji wa Simba, Lamine Moro ni mchezaji halali wa timu hiyo kwa sababu alikamilisha taratibu za usajili.
Taarifa iliyotolewa jana na Kamati ya mashindano ya SportPesa ilisema kuwa mshambuliaji huyo raia wa Ghana ni mchezaji halali wa Simba ambaye alisajiliwa na TFF tangu Januari 15 mwaka huu na kupewa leseni ya muda yenye namba 002821M94.
Mechi nyingine ya hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuwakutanisha Mbao FC ya jijini Mwanza dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya.
MaoniMaoni Yako