Simba yaitaka Everton

Simba yaitaka Everton


Mabingwa watetezi hao wa Ligi Kuu Bara, wamepata ushindi huo katika Uwanja wa Taifa, wakitoka kupigwa mabao 5-0 ugenini dhidi ya AS Vita ya DR Congo, kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa matokeo hayo ya jana, sasa Simba itahitaji kushinda nusu fainali dhidi ya Bandari FC ya Kenya katika mechi ya hatua ya nusu fainali ya pili ambayo itachezwa kesho, ili kuendelea kuweka matumaini ya kucheza dhidi ya Everton ya England.
Mechi nyingine ya hatua ya nusu fainali itakuwa kati ya wababe wa Yanga, Kariobangi Sharks dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza.
Mbao ilitinga hatua hiyo baada jana nayo kuwavua ubingwa, Gor Mahia ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-3 kutokana na kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika ya 90 za kawaida.
Bingwa wa michuano hiyo hupata fursa ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Everton ambayo nayo hudhaminiwa na Kampuni ya SportPesa kama ilivyo kwa Simba, Yanga na Singida United kwa hapa nchini.
Katika mechi ya jana, bao la kwanza la Simba lilifungwa dakika ya 13 na Mganda Emmanuel Okwi aliyemalizia krosi safi iliyopigwa na beki raia wa Ivory Coast, Zana Coulibaly.
Dakika ya 48 Mzambia, Clatous Chama, alifunga bao la pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Okwi aliyekuwa ndani ya 18.
Bao la AFC Leopards lilifungwa na Vicent Oburu dakika ya 61 baada ya kuwachekesha mabeki wa Simba na kipa wao, Manula akawa ameshapotea na kupiga shuti lililoingia moja kwa moja wavuni.
Simba ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Hata hivyo, wageni AFC Leopards ndio walikuwa wa kwanza kufanya shambulizi kupitia kwa Mukangula Eugene, lakini akiwa jirani na lango la Simba alipiga pembeni wakati Simba ilikaribia kupata bao lingine dakika ya 19 kupitia kwa Okwi ambaye shuti lake lilidakwa na kipa Mkenya, Adira Jairus.
AFC walifanya shambulizi lingine kupitia kwa Wayela Tutawe, lakini beki wa Simba, Pascal Wawa, alimzuia vema na hivyo mpira kudakwa kirahisi na kipa, Manula.
Simba: Aishi Manula, Rashid Juma, Zana Coulibaly, Lamine Moro/Meddie Kagere (dk. 46), Pascal Wawa/Juuko Murshid (dk. 46), Jonas Mkude/James Kotei (dk. 46), Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Hunlede Kissimbo, Emmanuel Okwi/Muzamil Yassin (dk. 66) na Clatous Chama.
MaoniMaoni Yako